HISTORIA FUPI YA UKIMWI DUNIANI KWA UJUMLA

Posted On September 14, 2007

Filed under Uncategorized

Comments Dropped leave a response

Mgonjwa wa kwanza mwenye dalili za UKIMWI alionekana Marekani mwanzoni mwa miaka ya 80. Wanaume mashoga wa miji ya San Francisco na New York walianza kupatwa na maradhi adimu kuonekana pamoja na kansa ambayo ilikuwa tabu kutibu kwa tiba yoyote. Punde kidogo ndipo ilipogunduliwa kirusi cha HIV ambacho ilikuja kuthibitishwa kuwa ndicho kisababishi cha ugonjwa wa UKIMWI. HIV ni kitu gani ? Kirusi cha HIV kinatoka kwenye kundi la virusi la lentivirus ambao wanatabia ya kushambulia na kuharibu kinga ya mwili wa kiumbe.Tabia nyingine ni kukaa kwa muda mrefu ndani ya mwili wa kiumbe pasipo kuonyesha dalili. Viumbe hawa hupatikana kwenye wanyama kama paka,farasi ,kondoo n.k.Ila aina ya lentivirus aliyevuta macho ya wanasayansi ni SIV(Simian Immuno deficiency Virus)ambaye anashambulia nyani. Imeshagundulika kuwa HIV ,kirusi kinachosababisha UKIMWI ni zao
la SIV.Mwaka 1999 ,wanasayansi wachunguzi wa chuo kikuu cha Alabama waligundua aina ya SIV ambayo inafanana kwa ukaribu sana na HIV.Aina hii ya SIV ilitoka kwa nyani wenye asili ya Magharibi ya Kati mwa Afrika.
Inaaminika kuwa nyani wawili wenye SIV tofauti waliambukizana na kufanya muunganiko wa virusi viwili kuwa kimoja ambacho kiliambukizwa kwa nyani wa tatu.Kirusi cha nyani wa tatu ndio kilichokuwa na uwezo wa kushambulia binadamu na kusababisha UKIMWI. Inaaminika kuwa kirusi hicho ndicho kilicho safiri kutoka kwa nyani kwa binadamu kwa njia mbalimbali kutokana na mahusiano ya wanyama na binadamu kama uwindaji n.k Mahusiano ya HIV na UKIMWI : Mtu anapoambukizwa HIV,virusi hivyo hukaa kwenye chembechembe nyeupe za damu zinazoleta kinga ya mwili.Chembechembe hizo huitwa CD4.Virusi hivi hushambulia na kuua chembechembe za CD4 na kusababisha kupungua kwa kinga ya mwili na hivyo kusababisha maambukizi ya magonjwa mwilini kirahisi na hivyo kusababisha ugonjwa wa UKIMWI. Mtu mwenye afya njema huwa na chembechembe za CD4 kati ya 500 na 1500 katika millilita moja ya damu.Ugonjwa wa UKIMWI unaanza kujitokeza pale chembechembe hizo zinapopungua na kufikia chini ya 200.   

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s